Skip to main content

Ban aitolea mwito tena Syria kukomesha ukandamizaji

Ban aitolea mwito tena Syria kukomesha ukandamizaji

Huku hali ya mambo ikiendelea kuchacha nchini Syria ambako makundi ya waandamanaji yakiendelea kudhibitiwa na vikosi vya dola, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kukomeshwa kwa vitendo vya utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji hao na kusisitiza haja ya kuheshimu uhuru wa wananchi kuandamana.

Kwa kuzingatia ripoti za vyombo vya habari kumekuwa na ukandamizwaji mkubwa unaofanywa na vikosi vya serikali vyenye shabaya ya kuwabana wananchi wanaojitokeza barabarani kwa ajili ya maandamano.Mamia ya watu wanaaarifiwa kupoteza maisha katika wiki chache zilizopita baada ya kushambuliwa na vikosi vya serikali ambavyo vinapinga maandamano hayo

Akijadilia hali hiyo, Ban amesema amerejelea wito wake kwa kuitaka Syria kuachana na matumizi ya nguvu na badala yake amesisitiza haja ya kufungua ukurasa wa majadiliano kwa ajili ya kufikia suluhu ya kudumu.