Mabadiliko ha hali ya hewa ni tisho kwa amani na usalama duniani

20 Julai 2011

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa changamoto kubwa kwa amani na usalama duniani . Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mkurugenzi mkuu wa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa Achim Steiner amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha madhara makubwa.

Naye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa huku hali mbaya ya hewa ikiendelea kuzua madhara ni bayana kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni tisho kwa amani na usalama wa kimataifa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter