Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yaendesha shindano ili kupata njia bora ya kukabiliana na unyanyapaa

UM yaendesha shindano ili kupata njia bora ya kukabiliana na unyanyapaa

Upigaji kura unaendelea kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa ni shabaya kusaka njia bora itayotumika kuendesha kampeni barani Ulaya ili kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ambao unatajwa kuwaathiri mamia ya watu.

Kwa kuzingatia ripoti za hivi karibuni,kila wanawake watatu wawili wameathiriwa na vitendo vya unyanyasaji duniani kote. Ili kupata njia muafaka ya uanzishwaji wa kampeni hiyo, nchi zipatazo 40 barani Ulaya zimeingia kwenye kinyang’anyiro zikianisha mipango na mikakati yake na kisha kutatangazwa washindi watatu.

Kwenye mabango ya upigaji kura kuna ujumbe unaosema ''PIGA KURA KUSEMA HAPANA-TUSHIKAMANE DHIDI YA UNYANYASAJI''. Shindano hilo limeandaliwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kwa Ulaya Magharibi ikishirikiana na taasisi nyingine kadhaa za Umoja huo.