Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashutumu vikali mashambulizi kwenye Ikulu ya rais wa Guinea

Ban ashutumu vikali mashambulizi kwenye Ikulu ya rais wa Guinea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la shambulizi lililofanywa katika makazi ya rais wa Guinea na wakati huo huo amewataka wananchi wa taifa hilo kujiweka kando na vitendo ambavyo vinaweza kuzika mchakato wa ukuzaji demokrasia.Ripoti zinasema kwamba Rais Alpha Conde hakujeruhiwa katika tukio hilo lilojiri alfajiri ya kuamkia jana katika mji mkuu wa Conakry.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Ban amesisitiza kwa kusema kuwa kuwepo kwa hali ya kutoelewana ama tofauti zozote hakuwezi kukadhihirishwa kwa vitendo vya ghasia.Ameitolea mwiyto jamii ya Guinea kujiepusha na matumizi ya nguvu ama kuibua vitendo vya uchochezi,ambavyo amedai kwamba vinakandamiza mchakato wa uimarishwaji wa demokrasia inayoanza kuchipua upo kwenye eneo hilo la afrika magharibi.