ICTY yakaribisha kukamatwa kwa Goran Hadzic

20 Julai 2011

Mahakama inayosikiliza kesi za ukiukaji wa haki za binadamu kwa iliyokuwa Yugoslavia ya zamani imekaribishwa kukamatwa kwa Goran Hadzic nchini Serbia mtoro ambaye amekuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka saba sasa. Hadzic ambaye alikuwa rais wa zamani kwenye eneo lililojitangaza huru la Serbia Krajina alifunguliwa mashtaka mwaka 2004 na mwendessha mashataka kutokana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita uliotekelezwa mashariki mwa Slavonia na Croatia kati ya mwaka 1991 na mwaka 92.

Hadzic ndiye mtoro wa mwisho aliyesalia kati ya watu 161 waliokuwa na mashtaka kwenye mahakama hiyo. Baada ya kusafirishwa kwenda kwa mahakama hiyo Hadzic atawekwa kizuizi akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake na anaruhusiwa kukata rufaa kwa kila shtaka lililo mbele yake.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter