Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuboresha huduma za kibindamu ni muhimu siku za usoni: Amos

Kuboresha huduma za kibindamu ni muhimu siku za usoni: Amos

Mratibu kwenye Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos amesema kuwa huku huduma za dharura za kibindamu zikitarajiwa kuongezeka kote duniani katika siku zijazo inahitaji kuboresha ushirikiano na kuchukua hatua za haraka wakati kunapohitajika.

Amos amesema kuwa changomoto zilizo duniani kama vile mabadiliko ya hali ya hewa , kupanda kwa gharama ya kawi na chakula, uhahamiaji , kuongezeka kwa haraka kwa idadi ya watu na kuharibika kwa mazingira ni masuala yanayoendelea kuchangia kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)