Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaitangaza hali kwenye pembe ya Afrika kuwa inayohitaji hatua za haraka

WFP yaitangaza hali kwenye pembe ya Afrika kuwa inayohitaji hatua za haraka

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP limesema kuwa watu milioni 11.3 wanahitaji misaada ya chakula kufuatia ukame unaoshuhudiwa kwenye pembe ya Afrika ambapo lataka kuchukuliwa kwa hatua za dharura na kuonya kuwa huenda hali hiyo ikaleta maafa zaidi. Mkurugenzi mtendaji wa WFP Josette Sheeran amesema kuwa WFP kupitia usaidizi wa mashirika mengine imekuwa ikitoa huduma kwa muda wa miezi sita iliyopita.

Sheeran amesema kuwa WFP inakaribisha tangazo la hivi majuzi kutoka kwa wale wanaosimamia shughuli kusini mwa Somalia la kuongezeka kwa huduma za kibinadamu kuwasaidia walioathirika zaidi ya umake. WFP na mashirika mengine ya kutoa huduma za kibinadamu yameshindwa kutoa huduma zao katika eneo la Kusini mwa Somalia tangu mwaka 2010 hali ambayo imechangia wanaoishi kwenye maeneo hayo kukosa usaidizi hasa watoto.