Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq yahitaji uungwaji mkono wa UM

Iraq yahitaji uungwaji mkono wa UM

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ad Melkert anasema kuwa taifa la Iraq linaweza kusherehekea hatua lililopiga lakini hata hivyo linakabiliwa na changamoto zikiwemo za kisiasa , kiusalama na za kimaendeleo zinazohitaji uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa jamii ya kimataiafa.

Akilihutubia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Melkert alitaja kati ya maendeleo yaliyopatikana kama vile kuandaliwa kwa uchaguzi na katiba ambayo inaruhusu kushiriki kwa wanawake kwenye siasa. Kupitia kwa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu huduma za ujumbe wa UM nchini Iraq UNAMI ni kuwa Iraq inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo inahitaji usaidizi wa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.