Chombo cha UM kinachohusika na utalii cha haidi kuiunga mkono India iliyokabiliwa na mashambulizi ya kigaidi

19 Julai 2011

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowajibika na usimamiaji wa utalii ameelezea masikitiko yake juu ya matukio ya vitendo vya ugaidi vilivyotokea wiki iliyopita katika mji wa India Mumbai, na ameiahidi kuendelea kuziunga mkono serikali za Kusini mwa Asia kukabiliana na hali kama hiyo.Makundi ya kigaidi yalidai kuhusika kwenye tukio hilo ambalo lilipoteza maisha ya watu kadhaa na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Taleb Rifai, amesema katika taarifa yake kuwa ameshtushwa mno na tukio hilo ambalo ameliita kuwa ni la kikatili. Amewatumia salama za rambi rambi familia zilizopoteza ndugu zao na kuwapa pole wale waliojeruhiwa.Amesema taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa itaendelea kuwa karibu na serikali ya India hasa katika kipindi hiki kigumu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud