Rais wa Baraza Kuu ataka kuwepo majadiliano zaidi juu ya mageuzi kwenye Baraza la Usalama

19 Julai 2011

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amezitaka nchi wanachama wa umoja huo kujiingiza kwa dhati kwenye majadiliano yanayoendelea sasa kuhusiana na mpango wa mageuzi ndani ya Baraza la usalama.Kuna majadiliano yanayopewa uzito ambayo yanataka kupanuliwa kwa chombo hicho na kukaribisha wanachama zaidi, tofauti na ilivyo sasa ambapo kina wanachama wachache.

Akizungumza kwenye kongamano linalojadilia mageuzi hayo huko Mexico, Rais Joseph Deiss amesema kuwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapaswa kujitokeza kujadiliana magauzi hayo na hatimaye kufukia kwenye shabaya ya pamoja.

Amesema hatma juu ya nchi ngapi ziwe wanachama kwenye Baraza la usalama inasalia mikononi mwa nchi 193 ambazo ni mwanachama wa umoja wa mataifa.Kwa hivi sasa Baraza la usalama linaundwa na nchi wanachama 15, lakini nchi tano tu ndizo wanachama wa kudumu zikihodhi mamlaka yote.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter