Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame unaoendelea katika Pembe ya Afrika umeathiri pia wafugaji:IOM

Ukame unaoendelea katika Pembe ya Afrika umeathiri pia wafugaji:IOM

Shirika la kimatifa la uhamiaji IOM linasema kuwa ukame unaoendelea kuathiri sehemu nyingi nchini Somalia , Kenya , Ethiopia na Djibout umesababisha watu kuhamia sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi zao.

Kuhama huku hakuwahusishi tu wakimbizi au watafuta hifadhi bali pia wafugaji ambao wanahama wakitumia njia zilizo ngumu kufahamika wakianzia vijijini kwenda mijini huku maelfu wakiwa mipaka na kuingia nchi zingine. Radio ya Umoja wa Mataifa imezungumza na Jumbe Omar Jumbe msemaji wa IOM.