Bokova alaani mauaji ya mwandishi wa habari nchini Mexico

19 Julai 2011

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kulinda uhuru wa vyombo vya habari amelaani mauaji ya mwandishi mmoja wa habari raia wa Mexico akisema kuwa hicho ni kisa cha hivi majuzi cha waandishi wanaouawa kwa sababu ya uhuru wa kusema. Angel Castillo Corona aliandika makala kuhusu siasa kwenye gazeti moja na baadaye watu wasiofahamika wakamvamia na kumpiga hadi akafa kwenye barabara ya kutoka Ocuilan kwenda Tiaguistenco kwenye kisa ambapo pia mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 16 aliuawa.

Irina Bokova mkurugenzi wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja swa Mataifa UNESCO amelaani vikali kuuawa kwa Castillo ambaye ni mwandishi wa tatu wa  habari kuuawa nchini Mexico kwa muda wa mwezi mmoja uliopita.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud