Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Armenia yaondosha vikwazo vya kusafiri kwa watu wenye HIV

Armenia yaondosha vikwazo vya kusafiri kwa watu wenye HIV

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa UKIMWI (UNAIDS) limekaribisha hatua iliyochukuliwa na serikali ya Armenia iliyoondosha marafuku ya kutosafiri kwa watu wenye virusi vya HIV. Armenia ilitangaza hapo jana kwamba kuanzia sasa inaondosha vikwazo vya kusafiri kwa watu wanaoshi na virusi vya HIV na hivyo kuingia kwenye hatua mpya inayoungwa mkono na jumuiya za kimataifa.

Kulingana na UNAIDS bado nchi nyingine 48 ambazo zinapiga marafuku kwa watu wenye virusi vya ugonjwa huo kuingia ama kuishi. Akizungumzia hatua hiyo ya Armenia Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Michel Sidebe pamoja na kuupongeza uamuzi huo lakini pia alizitolea mwito nchi nyingine ambazo zinazoendelea kukumbatia sheria ya aina hiyo. Amezitaka ziondoshe mwenendo huo.