Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasayansi wakutana Geneva kujadili biashara ya wanyama wa majini na ngozi za wale wanaotambaa

Wanasayansi wakutana Geneva kujadili biashara ya wanyama wa majini na ngozi za wale wanaotambaa

Wanasayansi kutoka kote duniani wanakutana mjini Geneva kunzia leo tarehe 18 hadi 22 kwa mkutano wa 25 wa kamati ya wanyama kuhusu wanyama walio kwenye hatari ya kuangamia. Karibu wajumbe 200 wanatarajiwa kuhudhuria, yakiwemo mashirika ya Umma na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Ajenda kuu kwenye mkutano huo itakuwa ni mjadala kuhusu familia ya samaki na ngozi za wanyama wanaotambaa ambapo huenda maeneo yakalindwa ikiwa idadi ya wanyama hao itapungua. Pia kamati hiyo itaangazia biashara ya kimataifa ya nyangumi. Mwaka uliopita bishara ya samaki wenye gharama ya juu iliruhusiwa kuendelea lakini hata hivyo kuna wasi wasi kuhusu hali ya nyangumi. Kamati hiyo pia itajadili matokeo ya warsha kuhusu nyoka iliyoandaliwa nchini China inayopendekezwa kusimamiwa kwa bishara ya ngozi ya nyoka.