Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya wanafunzi walio na nia ya kuchukua uongozi wa UM wa mfano

Mafunzo ya wanafunzi walio na nia ya kuchukua uongozi wa UM wa mfano

Vijana 19 wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi 17 wanachama wa Umoja wa Mataifa walikutana hapa New York kwenye makao makuu ya UM kwa ajili ya mafunzo maalumu ya kuchukua jukumu la uongozi wa Umoja wa Mataifa wa Mfano yaani UN Model.

Wanafunzi hao kutoka Australia, Bolivia, Brazil, China, Canada, Ecuador, Ufaransa, Ujerumani, Indonesia, Lebanon, Mexico, Peru, Macedonia, Jamhuri ya Korea, Urusi, Kenya na Uganda wataongoza mkutano wa mfano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa wakijadili mada mbalimbali huko Korea ya Kusini.

Uongozi huo ulio na Katibu Mku, naibu Katibu Mkuu na wawakilishi mbalimbali una lengo la kuchagiza mchango wa vijana katika maendeleo ya nchi zao ikiwemo kuleta amani. Na mada kuu ya mkutano wao mwezi ujao ni maendeleo endelevu sambamba na kulinda mazingira. Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na Abdala Salim mwanafunzi wa sheria kutoka chuko kikuu cha Naironi na Julie Farzana kutoka chuo kikuu cha Amerikani(USIU) mjini Nairobi ambao kwanza wanafafanua kilichowaleta.

(MAKALA UN MODEL BY FLORA NDUCHA)