Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na polisi nchini Haiti katika oparesheni ya kupambana na uhalifi mjini Port-au- Prince

UM na polisi nchini Haiti katika oparesheni ya kupambana na uhalifi mjini Port-au- Prince

Umoja wa Mataifa na idara ya polisi nchini Haiti wamezindua oparesheni ya pamoja ya kupambana na uhalifu katika maeneo muhimu kwenye mji mkuu Port-au- Prince. Zaidi ya wanajeshi 2,100 wametumwa kwenye maeneo matatu kama sehemu ya oparesheni hii iliyo na lengo la kuusaidia utawala nchini Haiti kutoa usalama na utulivu kwenye mji wa Port-au-Prince.

Kamanda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti meja Luiz Ramos amesema kuwa mara wakati oparesheni hiyo itakapokamilika wataandaa shughuli kadha kwa ushirikiano na wananchi kama vile kuondoa taka kutoka mitaa ya mji na kuimarisha barabara.