Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watoto 2000 wa Gaza watia fora kwenye michezo ya kiangazi

Zaidi ya watoto 2000 wa Gaza watia fora kwenye michezo ya kiangazi

Zaidi ya watoto 2000 wa Gaza wamechukua tukio la kihistoria duniani pale waliposhiriki kikamilifu kwenye michezo mbalimbali iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kama sehemu ya michezo ya majira ya kiangazi. Taarifa zinasema kuwa watoto hao walivunja rekodi ya dunia kwa kushiriki kikamilifu kwenye michezo hiyo iliyofanyika eneo lijulikanalo Kherbit El-Addas, Rafah ambalo lipo karibu na Khan Younis.

Akiwapongeza watoto hao kutokana na mafanikio hayo, Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utoaji wa misaada ya kiutu kwa Palestina UNRWA, Christer Nordahl alisema kuwa mafanikio hayo ni jambo la kujivunia.Kwa kipindi cha miaka mitano sasa UNRWA huandaa michezo ya majira ya kiangazi inayohusisha soka, sanaa na shughuli nyinyine mbalimbali.