Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya UM kuanza kukusanya silaha Ivory Cost

Vikosi vya UM kuanza kukusanya silaha Ivory Cost

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Cost vitaanza kukusanya masalia ya silaha ndogondogo katika eneo la Yopougon, lililopo kando kando ya mji mkuu wa Abijan silaha ambazo zilizotolewa kwa hiari na askari.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa DDR kitengo kinachohusika masuala ya silaha hatua hiyo inalenga kulisafisha eneo la Yopougon.Bi Sophie Da Camara amewatolewa mwito pia wale wanaoendelea kumiliki silaha kuzisalimisha mara moja.Amesema zoezi hilo linatazamiwa pia kufanywa katika maeneo yote ya Ivory Cost.Mkwamo wa kisasi uliodumu kwa kipindi cha miezi kadhaa ulifikia kikomo baada ya kutiwa nguvuni kwa rais aliyeng’ang’ania madaraka Laurent Gbagbo.