Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za kuwasidia wahamiaji nchini Libya zaendelea

Jitihada za kuwasidia wahamiaji nchini Libya zaendelea

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa wahamiaji wanaokimbia mapigano nchini Libya wanaishi kwa hofu na kwa sasa linaendelea kuhamisha idadi kubwa ya wakimbizi inayozidi kuuongezeka nchini Libya. Msemaji wa IOM Jemini Pandya anasema kuwa karibu wahamiaji 625,000 kwa sasa wameikimbia Libya tangu mwishonmi mwa mwezi Februari akiongeza kuwa wane wana hofu na hawawezi kuondoka.

(SAUTI YA JAMINI PANDYA)

“Leo, wakati tunapowahamisha wahamiaji 230 kutoka Misrata ambao wako njiani kwenda Benghazi, tunaendelea kupokea ripoti za wahamiaji zaidi na zaidi waliotawanyika kote nchini na ambao hawawezi kuondoka. Wahamiaji hao wanaaminika kuwa kwenye sehemu kadha wengi wao wakiwa wamejificha kwa sababu hawana uwezo wa kuondoka Libya na kurudi nyumbani.”

IOM inasema kuwa imepokea ripoti kuwa karibu wahamiaji 1000 wamejificha karibu na mji wa Kufra kusini mashariki mwa Libya huku wengine 3000 wakiwa katika eno linalouzunguka mji ulio kusini wa Sebha.