Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakaribisha hatua ya Kenya ya kupanua kambi ya wakimbizi ya Dadaab

UNHCR yakaribisha hatua ya Kenya ya kupanua kambi ya wakimbizi ya Dadaab

Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres amepongeza tangazo la serikali ya Kenya kuwa itafungua kambi ndogo ya Ifo Two iliyo kwenye kambi ya Daadab karibu na mpaka kati ya Kenya na Somalia.

Takriban wakimbizi 1300 wamekuwa wakiwasili kila siku nchini Kenya wakikimbia mapigano nchinin Somalia. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa kufunguliwa kwa kambi hiyo kutasaidia kupunguza msongamano ulio kwenye kambi ya Daadab.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS )