Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia wakutana kujadili hali nchini Libya

Viongozi wa dunia wakutana kujadili hali nchini Libya

Wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO wamefanya mkutano wao wa nne kuhusu Libya mjini Istanbul nchini Uturuki katika juhudi za kupata suluhu kwa mzozo unaondelea kwenye taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika. Hili linajiri wakati mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yakiingia mwezi wake wa tano. Umoja wa Mataifa unataka kuwe na makubalino ya kisiasa ukisema mzozo huo hautatatuliwa kwa njia ya kijeshi.

Umoja wa Mataifa unataka viongozi wanaokutana mjini Istanbul kuunga mkono jitihada za mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ili kuiwezesha serikali na wanaopigania mabadiliko kufanya mazunguzmo. Wakati huo huo hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Libya wakati kunaposhuhudiwa uhaba wa chakula , mafuta pamoja na madawa na pia ukosefu wa maji.