Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali bado mbaya kwenye pembe ya Afrika WHO

Hali bado mbaya kwenye pembe ya Afrika WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa kutokana na kuwepo kwa huduma duni za kiafya kwenye maeneo yanayokumbwa na ukame , hali duni ya kutoa chanjo , kuhama kwa watu na ukosefu wa mji safi pamoja na usafi, sasa kuna hatari kutokea maambukizi ya magonjwa.

Wanasema kuwa lengo la sekta ya kiafya ni kushughulikia hali mbaya ya utapiamlo iliyopo sasa , magonjwa ya watoto , afya ya akina mama, utoaji wa chanjo na kuzuia magonjwa yanayotokana na maji. WHO inasema kuwa sekta ya afya imetengewa fedha kidogo wakati ambapo mahitaji ya kuwapa huduma za dharura watoto wanaosumbuliwa na utapiamlo yakiongezeka. Tarik Jasarevic kutoka WHO anasema kuwa shirika hilo linachukua hatua za kusaidia hali hiyo na pia kuwapa mafunzo wahuduma wa afya.