Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yatangazwa kuangamiza ugonjwa wa Pepopunda

Uganda yatangazwa kuangamiza ugonjwa wa Pepopunda

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limepongeza juhudi za Uganda baada ya kuwa taifa la 20 tangu mwaka 2000 katika kuangamiza ugonjwa wa pepopunda. UNICEF linasema kuwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ulilenga wilaya 25 nchini Uganda na kutoa chanjo kwa karibu wanawake milioni mbili walio na umri wa kuzaa kati ya mwaka 2002 na 2009.

Watoto wanaozaliwa wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa Pepopunda ikiwa hawatahudumiwa kwa njia inayofaa au ikiwa watahudumiwa kwa njia za kitamaduni .