Ban ataka mashirikiano zaidi ili kufikia shabaya ya amani

Ban ataka mashirikiano zaidi ili kufikia shabaya ya amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa watu wenye utashi wa amani wanayo nafasi kubwa kuunga mkono kampeni ya umoja huo juu ya ufikiaji wa shabaya ya amani na maendeleo.Ban ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na magwiji wa taaluma ya habari alipokutana nao New York.

Amesema Umoja wa Mataifa unahitaji ushirikiano toka kwa watu wa kanda mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wanaharakati, maafisa watendeaji ikiwemo pia viongozi wa dini ili kufikia dhamira ya uimarishwaji wa hali ya amani duniani kote.Ama alizungumzia nafasi yake kwenye Umoja huo akisema kuwa anaona ni mtu aliyepewa heshima kubwa kuongoza taasisi hiyo .