Kuna haja ya kuwepo kwa mipango endelevu ili kusunuru janga la njaa katika eneo la Pembe ya Afrika-UM

Kuna haja ya kuwepo kwa mipango endelevu ili kusunuru janga la njaa katika eneo la Pembe ya Afrika-UM

Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya usalama wa chakula wamesema kuwa hatua za dharura kwa ajili ya kukabili tatizo la ukame katika eneo la Pembe ya Afrika, lazima ziende sambamba na uanzishwaji wa mipango ya muda mrefu ili kuzikabili changamoto za mara kwa mara.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwataka wajumbe kwenye mkutano huo uliohusisha maafisa wa ngazi za juu, kuangazia kwa karibu hali inavyozorota kwenye eneo hilo na kisha kuanisha njia ya kukabili janga hilo.Akizungumza zaidi kwenye mkutano huo, Ban alitaka mipango hiyo iende sambamba kwa mustakabali unaojali nishati na suala la tabia nchi.

Nguvu kazi hiyo iliyoundwa, inajumuisha wakuu 20 wa idara mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Wajumbe kwenye nguvu kazi hiyo kadhalika walijadilia kwa kina juu ya kuwepo haja ya kuwainua wakulima  wadogo hasa zaidi wanawake walioko kwenye nchi zinazoendelea.Zaidi ya watu milioni 11 walioko katika eneo la Pembe ya Afrika wanakabiliwa na mkwamo wa janga la njaa.