Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabomu yaliyoimarishwa yasababisha vifo zaidi vya raia nchini Afghanistan

Mabomu yaliyoimarishwa yasababisha vifo zaidi vya raia nchini Afghanistan

Ripoti mpya kutoka Umoja wa Mataifa inasema kuwa raia wengi zaidi wanaendelea kuuawa nchini Afghanistan na kundi la Taliban na makundi mengine ya wanamgambo yanayotumia mabomu yaliyoimarishwa.

Ripoti kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA inaonyesha kuongezeka kwa asilimia 15 kwa watu waliouawa kutoka mwaka uliopita huku Taliban na makundi mengine yakichangia asilimia 80 ya vifo hivyo. Mkurugezni wa haki za binadamu kwenye ujumbe wa UNAMA Georgette Gagnon anasema kuwa mabomu hayo huwa yanalipuka wakati yanapohisi uzito kidogo.