Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Antony Lake ziarani nchini Kenya

Antony Lake ziarani nchini Kenya

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Antony Lake yuko nchini Kenya ambapo anatarajiwa kuzipa msukumo shughuli za mashirika ya Umoja wa Mataifa yanapojitahidi kuokoa maisha kutokana na janga la njaa linalotishia maisha ya mamilioni ya watu wengi wakiwa ni watoto. Janga hilo limechochewa zaidi na ukame wa muda mrefu , kupanda kwa bei ya vyakula na mzozo uliopo nchini Somalia.

Takriban watoto 500,000 nchini Somalia, Ethiopia na Kenya kwa sasa wanakabiliwa na hali mbaya ya utapia mlo. Wakati wa ziara hiyo bwana Lake atafanya mikutano na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kabla ya kusafiri hadi eno la Turkana, wilaya kame iliyo Kaskazini magharibi mwa Kenya iliyo na watu 850,000 wengi wakiwa ni wafugaji.