Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waikaribisha Sudan Kusini kuwa mwanachama wake 193

UM waikaribisha Sudan Kusini kuwa mwanachama wake 193

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limelikubali taifa la Sudan Kusini kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Uhuru wa Sudan Kusini kutoka Sudan umetokana na kura ya maoni ya Januari mwaka huu iliyoandaliwa chini ya makubaliano ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Sudan kusini. “Kwa wakati huu , mahala hapa , ulimwengu unakusanyika na kusema kwa pamoja” amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban- Ki moon.

Ban ambaye pia alihudhuria sherehe za uhuru wa taifa hilo mjini Juba Jumamosi iliyopita amesema kuwa UM utaendelea kuisaidia Sudan Kusini inapojaribu kujiimarisha. Ban ameongeza kuwa ni lazima Sudan na Sudan Kusini washirikiane ili waweze kunufaika.

Bendera ya Sudan Kusini sasa iko juu ya mlingoti pamoja na bendera zingine za wanachama wa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.