Sudan yamwachilia mmoja wa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa

13 Julai 2011

Utawala nchini Sudan umemwachilia mfanyikazi mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyekamatwa mwezi mei mwaka huu kwenye jimbo linalokumbwa na mzozo la Darfur, lakini hata hivyo mfanyikazi mwingine wa Umoja wa Mataifa bado anaendelea kubaki kizuizini. Hawa Abdalla Mohamed mfanyikazi wa kikosi cha pamoja cha kulinda ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika nchini Sudan UNAMID aliachiliwa hii leo mjini Khartoum.

Bi Mohamed alikamatwa tarehe 6 mwezi mei nyumbani kwake kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Shouk karibu na El Fasher mji mkuu wa la Darfur Kaskazini. Mwenzake Idriss Abdelrahman aliyekamatwa mwezi Aprili bado anazuiliwa kwenye mji wa Nyala ambao ni mji mkuu wa Darfur Kusini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter