Skip to main content

UNESCO yazindua mpango wa kutoa taarifa za dharura wakati wa kujiri majanga ya kimaumbile Kusini mwa Asia

UNESCO yazindua mpango wa kutoa taarifa za dharura wakati wa kujiri majanga ya kimaumbile Kusini mwa Asia

Ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuipiga jeki Pakistan ili kukabiliana na majanga ya tabia nchi,shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni,UNESCO limezindua mpango maalumu ambao utawezesha kutoa taarifa za tahadhari mapema kabla ya kujiri kwa janga.

Mpango huo ambao pia umehusisha mashirika mengine kadhaa unatazamiwa kutoa msaada wa dharura kwa mataifa yaliyoko katika eneo la Kusin mwa Asia.Nchi hizo katika kipindi cha mwaka uliopita, zilikubwa na majanga ya kimaumbile yaliyosababisha uharibifu mkubwa.Mpango huo ambao unasimamiwa kwa karibu na UNESCO kwa kushirikiana na serikali za Pakistan na Japan unalenga zaidi kupunguza maafa kwa binadamu pamoja na maeneo mengine ya kiuchumi.