Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha makubaliano yenye shabaya ya kuongeza uzalishaji wa ARVs kwa nchi maskini

UM wakaribisha makubaliano yenye shabaya ya kuongeza uzalishaji wa ARVs kwa nchi maskini

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI limekaribisha kwa furaha makubaliano yaliyofikiwa baina ya mamlaka ya kitabibu na makampuni ya kifamasia ambayo yamekubaliana kuongeza usambazaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.

Kwa mujibu wa shirika hilo UNAIDS, makubaliano hayo ambayo ni ya kwanza kufanywa yanafungua ukurasa mpya unaoonyesha namna mashirika ya binafsi yanavyoanza kutilia uzito wa pekee suala la UKIMWI.Katika makubaliano hayo pande zote zimeridhia kuachiana uhuru wa haki miliki hatua ambayo itasaidia uzalishaji na usambazaji wa vidonge hivyo vya ARVs.Makampuni ambayo yatavutiwa na utengenezaji wa dawa hizo kwa ajili ya kujisambaza katika nchi zinazoendelea sasa zitaruhusiwa kufanya hivyo bila masharti yoyote.