Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya nishati mbadala yazidi kuongezeka duniani

Matumizi ya nishati mbadala yazidi kuongezeka duniani

Ripoti ya kila mwaka kuhusu matumzi ya nishati mbadala mwaka 2011 iliyotolewa hii leo inaonyesha kuwa sekta ya nishati mbadala inaendelea kukua hata baada ya kuwepo hali mbaya ya uchumi.

Ripoti hiyo inasema kuwa mwaka 2010 nishati mbadala ilichangia asilimia 20 ya uzalishaji wa kawi kote duniani huku nishati hiyo ikichangia karibu robo ya nishati inayotumika kote duniani.Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa kwa sasa watu wengi zaidi huwa wanatumia nishati mbadala na idadi hiyo inazidi kuongezeka.