Sudan Kusini kuwa mwanachama wa 193 wa Umoja wa Mataifa

13 Julai 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubali taifa la Sudan Kusini kuwa mwanachama wake . Kitachofuata sasa ni kwamba Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litapiga kura ili kuifanya Sudan Kusini mwanachama wa 193 wa Umoja wa Mataifa.

Sudan Kusini ilitangazwa rasmi kuwa taifa huru kutoka Sudan Julai 9 mwaka huu baada ya vita vya miaka mingi kati ya nchi hizo mbili. Makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar anasema kuwa nchi yake imejitolea kufuata kanuni za UM lakini inatambua changamoto zilizo kati yake na jirane wake Sudan.

(SAUTI YA RIEK MACHAR)

Hata hivyo bado kuna ukosefu wa usalama kwenye maeneo ya mpaka moja yao likiwa eneo la Abyei ambalo linahitajika kupiga kura ya kuamua ikiwa litajiunga na Sudan Kusini au litasalia Kaskazini.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter