Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP una mpango wa kurejesha huduma zake nchini Somalia

WFP una mpango wa kurejesha huduma zake nchini Somalia

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linasema kuwa huku kukiwa na mahitaji makubwa ya huduma Kusini mwa Somalia kwa sasa linafanya mipango na mratibu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia kutafuta ya kurejesha huduma zake na iwapo tu usalama wa kutosha utatolewa.

WFP iliondoka kwenye maeneo yanayokaliwa na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia mapema mwaka 2010 kufuatia hatari iliyokuwa ikiwakabili wafanyikazi wake, pamoja na vizingi vilivyowekwa vikiwemo vya kulipa kodi isiyohitajika. Hata hivyo WFP imekuwa ikiendesha huduma zake mjini Mogadishu , katikati na Kaskazini mwa Somalia kwa kutoa chakula kwa watu milioni 1.5.