Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali na Shule zatajwa kuwa salama kwa watoto

Hospitali na Shule zatajwa kuwa salama kwa watoto

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa hospitali na shule sasa ni makao salama kwa watoto . Kwenye azimio lililopitishwa hii leo, baraza la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa yeyote ambaye atashambulia vituo hivyo. Shule zimekuwa zikilengwa kwenye mashambulizi kutoka kwa vikosi vya serikali na visivyo vya serikali kwa karibu nchi 31 barani Afrika , Asia, Ulaya , Amerika Kusini pamoja na mashasriki ya kati.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Antony Lake amepongeza uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa na kuutaja kama hatua ya kumaliza ukwepaji wa sheria.