Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vizuizi vya Israeli kwa Palestina vinaleta taswira mbaya: UM

Vizuizi vya Israeli kwa Palestina vinaleta taswira mbaya: UM

Ikiwa imepita miaka 7 sasa tangu mahakama ya kimataifa kutamka kuwa kitendo kilichofanywa na Israel cha kuweka vizuizi kwenye eneo inalikalia la Palestina kuwa ni kitendo kilichoenda kinyume na sheria, ripoti moja ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa jamii ya watu walioko upande wa mashariki mwa mji wa Jerusalem wameendelea kutengwa.

Ripoti hiyo imefahamisha kuwa jamii ya wakazi wa ukanda wa Gaza wamenyimwa fursa ya kuchangamana na mji mzima wa Jerusalem baada ya kutenganishwa na kizuizi cha ukuta kilichowekwa na Israel.Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya usamaria mwema OCHA wananchi wa Palestina walioko kwenye eneo hilo wamepewa masharti kupitia kwenye maeneo ya ukaguzi na kwa ajili ya kwenda kufuata huduma za kijamii kama elimu, matibabu na kwenye manunuzi.

Ripoti hiyo pia imefafanua matatizo ya kilimo yanayowakumba wakulima wa Palestina kutokana na kizuizi hicho