Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha hatia iliyochukuliwa na serikali ya Chad kutengua mpango wake wa kumrejesha kwao rais wa zamani wa Chad

Pillay akaribisha hatia iliyochukuliwa na serikali ya Chad kutengua mpango wake wa kumrejesha kwao rais wa zamani wa Chad

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu amesema ameunga mkono na kukaribisha uamuzi wa serikali ya Senegal iliyobadilisha uamuzi wa kumrejesha kwao rais wa zamani wa Chad Hissène Habré.Hapo jana Senegal ilisema kuwa leo ingemsafirisha hadi kwao rais huyo wa zamani wa Chad ambaye hata hivyo alikuwa amehukimiwa adhabu ya kifo na mahaka ya nchini kwake wakati akiendelea kuishi uhamishoni.

Hata hivyo Navi Pillay ametoa zingatio akisema kuwa kutorejeshwa nyumbani kwa kiongozi huyo hakuwezi kwenda sambamba na kupatiwa kinga ya kutofikishwa mbele ya mkono wa sheria.Pillay aliitaka Senegal kutengua uamuzi wa kumrejesha nyumbani kiongozi huyo kwa kile alichoeleza wasiwasi wa kukosekana kwa usalama na mfumo hafifu wa uendeshwaji wa mashtaka.