UNHCR yatoa usaidizi kwa wanaokimbia ghasia kaskazini magharibi mwa Pakistan

12 Julai 2011

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linafanya jitihada za kuwasaidia watu wanaokimbia mapigano katika eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan. Mapigano hayo yaliyoanza mwezi uliopita yamewalazimu watu kukimbia makwao kwenye vijiji nane katika eno hilo huku utawala wa eneo hilo unaamini kuwa karibu watu 84,000 wamekimbia makwao kufuatia mapigano hayo . Kwa muda wa majuma mawili yaliyopita zaidi ya familia 700 zimetafuta hifadhi kwenye kambi mpya iliyobuniwa katika eno la Durrani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter