12 Julai 2011
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewaokoa zaidi ya watu 230 na watu wengine zaidi ya 40 waliojeruhiwa kutoka mji wa Misrata nchini Libya wakati mzozo kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika unapoendelea. Wahamiaji hao wanaopelekwa mji wa Benghazi wengi wao wanatoka nchini Niger na wengine nchini Chad , Ghana , Nigeria , Nepal , Bangladeshi na Yemen.
Wahamiaji 232 wengi wao vijana wa kiume wamekuwa wakiishi kwenye makao ya chama cha mwezi mwekundu nchini Libya ambapo idai yao imekuwa ikiongezeka. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.
(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)