Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maeneo kadha yakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Yemen: WFP

Maeneo kadha yakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Yemen: WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa kulingana na utafiti ulioendeshwa kwenye mikoa minne isiyo na usalama wa chakula nchini Yemen, unaonyesha kuwa uhaba wa chakula unazidi kuongezeka. Kwa sasa familia nyingi zinajaribu kubuni mbinu za kuishi katika hali hiyo kama vile kutumia fedha za matibabu kununua chakula na kuuuza mali.

Bei ya unga , Sukari na maziwa imepanda kwa kati ya asilimia 40 na 60 huku bei ya mkate ikiongezeka kwa asilimia 50 wakati ambapo pia kunashuhudiwa uhaba mkubwa wa mafuta. Wakati huo huo shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa watoto 72 wameuawa na 130 kujeruhiwa kwa risasi nchini Yemen wakati wa ghasia zilizoshuhudiwa nchini humo.