Mpango wa kuijumuisha Sudan Kusini kwenye Umoja wa Mataifa waanza

12 Julai 2011

Mpango ulio na lengo la kujumuishwa kwa taifa jipya la Sudan Kusini kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa umengo’a nanga baada ya rais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwasilisha ombi la Sudan kusini kwa idara zilizo na jukumu la kushugulikia ombi kama hilo.

Awali Kamati inayohusika na kujumuishwa kwa wanachama wapya kwenye Umoja wa Mataifa ilikutana kuangalia ombi hilo lililowasilishwa na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir tarehe 9 mwezi huu wakati nchi hiyo ilipopata uhuru wake .

(SAUTI YA NJOGOPA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter