Wategua mabomu wauawa Afghanistan

11 Julai 2011

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA unaripoti kuwa raia wanne wa Afghanistan ambao ni wafanyakazi wa kuondoa mabomu ya ardhini na vifaa vingine vya kivita vinavyolipuka wameuawa kwenye mkoa wa Farah nchini humo.

Ripoti zinasema kuwa wategua mabomu hao walitekwa pamoja na watu wengine 31 tarehe 6 mwezi huu ambapo walitambuliwa na kuuawa. UNAMA inasema kuwa mashambulizi dhidi ya watu wanaofanya kazi ya kuokoa maisha ni kitu ambacho hakitakubalika na imeitaka serikali kuchunguza kisa hicho na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter