Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eneo la Asia ya Kati latakiwa kuzingatia matumizi endelevu ya maji ya mto Amu Darya

Eneo la Asia ya Kati latakiwa kuzingatia matumizi endelevu ya maji ya mto Amu Darya

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limesema kuwa uimarishwaji wa mashirikiano ya dhati baina ya mataifa yanayotumia maji ya mto Amu Darya ambao ndiyo mto mrefu zaidi katika eneo la Asia ya Kati, kunaweza kuwa ndiyo sulihisho la kuduma juu ya hali ya amani na usalama kwenye eneo hilo.

Katika ripoti yake iliyozinduliwa hii leo, UNEP imesema kuwa mipango ya maendeleo  itakayotumia kiwango kikubwa cha maji inayokusudiwa kuchukuliwa inaongeza hali ya wasiwasi kwenye tatizo la tabia nchi, lakini hali hiyo inaweza kuepukwa kwa mafanikio makubwa kama nchi husika zitaleta pamoja utashi wao maelewano na mashirikiano.

Nchi za Afghanistan,Tajikistan,Turkmenistan na Uzbekistan ndiyo watumiaji wakumbwa wa maji na zinalaumiwa kutokana na matumizi yasiyozingatia dhana ya maendeleo endelevu.Katika ripoti yake hiyo, shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaweza zingatia juu ya utumizi wa rasimali ya maji katika hali ambayo kunafaidia pia mazingira ya wakati huu na yajayo.