Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Senegal kutafakari upya uamuzi  wa kutaka kumrejesha kwao kiongozi wa zamani wa Chad

UM waitaka Senegal kutafakari upya uamuzi  wa kutaka kumrejesha kwao kiongozi wa zamani wa Chad

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu ameelezea masikitiko yake kufuatia tangazo lililotolewa na serikali ya Senegal juu ya kusudio lake la kutaka kumtimua nchini humo rais wa zamani wa Chad Hissène Habré ambaye atarejeshwa nchini kwake alikokwisha hukumiwa adhabu ya kifo wakati akiendelea kuishi uhamishoni.  Mamlaka za Senegal zinaarifiwa kuwa na mazungumzo na maafisa wa serikali wa Chad na kukubaliana kiongozi wa zamani atarejeshwa nchini mwake hapo kesho.

Juu ya hatua hiyo, Kamishna Navy Pillay ameitaka serikali ya Senegal kutafakari upya hatua yake hiyo na akasisitiza kuwa  iwapo itapenda kuendelea na mpango wake huo basi lazima ihakikishe mazingira ya haki na ukweli yanapatikana.Pillay ameonyesha wasiwasi wake akisema kuwa kumrejesha kiongozi wa zamani katika mazingira ambayo siyo mjarabu kwa jambo lolote kunaweza kuchochea hali ya uvunjifu zaidi wa sheria za kimataifa.