UM kutoa misaada ya kitabibu kwa manusura wa ajali ya ndege Congo

11 Julai 2011

Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuhaidi kutoa msaada wa kitabibu kwa manusuru wa ajali ya ndege iliyoanguka mwishoni mwa juma katika mji wa Kisangani ambako watu kadhaa walipoteza maisha.

Katika taarifa yake, kikosi cha ulinzi wa amani nchini humo MONUSCO imesema kuwa Umoja wa  Mataifa utaendelea kuwa bega kwa geba na serikali ili kufanikisha utoaji wa huduma za dharura kwa manusura wa tukio hilo.Tayari maafisa wa shirika la afya ulimwenguni WHO wameanza kufanya kazi na mabwana afya wa serikali kwa ajili ya kuwahudumia waathirika hao.Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa  ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 112, ilianguka katika uwanja wa ndege wa Kisangani. Watu 50 walipoteza maisha katika tukio hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter