Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sidibe ziarani nchini China

Sidibe ziarani nchini China

Naibu waziri mkuu nchini China Li Kegiang amesema kuwa malengo matatu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la UNAIDS ya kuyafanya kuwa sufuri masuala yakiwemo maambukizi ya virusi vya ukimwi, ubaguzi na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa ukimwi kote duniani ni kama mwongozo kwa jitihada za kupambana na ugonjwa wa ukimwi nchini China. Akikutana na mkurugezni mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe, Li amesema kuwa hizi sufuri tatu ndilo lengo la China na China imejitolea kutekeleza masuala hayo.

(SAUTI YA MAUREEN KOECH)