Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama labuni ujumbe mpya Sudan Kusini

Baraza la Usalama labuni ujumbe mpya Sudan Kusini

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kulinda amani Alain Le Roy naye amesema kuwa hii ni njia ya kumaliza kazi iliyoanza kwenye makubalino ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe . Amesema kuwa umekuwa wakati mgumu wa miaka 6 ambao UNAMIS ilifanikiwa kuzuia kurejea tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kusaidia pande zote mbili.

Siku moja baada ya Sudan Kusini kutangazwa huru, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kubuni ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa utakaolisaidia taifa hilo jipya kuwa na amani na kuweka msingi dhabiti wa maendeleo pamoja na kuzuia mizozo na ukuaji wa uchumi. Ujumbe huo utaongozwa na mwakilishi mpya maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Hilde Johnson ambaye alimweleza haya Reem Abaza wa idhaa hii.