Afrika yapata taifa jipya la Sudan Kusini

Afrika yapata taifa jipya la Sudan Kusini

Jumamosi hii Julai 9 mwaka 2011 ni siku itakayoingia katika vitabu vya historia kote duniani baada ya machafuko ya takriban miongo miwili hatimaye moja ya nchi kubwa kabisa barani Afrika Sudan inagawanywa rasmi mapande mawili Kaskazini inayosalia kuwa Sudan na taifa jipya linalozaliwa Sudan Kusini. Umoja wa Mataifa , Jumuiya ya kimataifa , Wahisani, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na dunia nzima imeelekeza macho na masikio Juba mji mkuu wa taifa la 54 barani Afrika na Sudan yote kwa jumla , kuona historia ikiandikwa lakini kubwa zaidi nini kitakachofuata baada ya kujitawala.

Umoja wa Mataifa umejiandaa vilivyo kuhakikisha usalama umedumishwa ukizingatiwa kuna changamoto nyingi katika taifa hilo lililosambaratika na machafuko ambapo hadi sasa suala la Kordofan Kusini na Abyei yaliyoko mpakani yanatia mashaka. Kuchambua kwa kina histotia hii, matarajio na changamoto , mkuu wa idhaa hii Flora Nducha amezungumza na Dr Salim Ahmed Salim anayeifahamu vilivyo historia ya Sudan, aliyewai kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Afrika na mpatanishi maalum wa Umoja wa Afrika katika mzozo wa Darfur.

(MAHOJIANO NA DR SALIMAHMED SALIM)

Ni Dr Salim Ahmed Salim akizunguumza na mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha kuhusu historia ya kuzaliwa taifa jipya la Sudan kusini.