Marekani imekiuka sheria za kimataifa kwa kumnyonga Leal Garcia: PILLAY

8 Julai 2011

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa Marekani imekiuka sheria za kimataifa baada ya kumyonga raia wa Mexico. Humberto Leal García alipewa hukumu ya kifo kwenye jimbo la Texas kufuatia makosa ya kuua mwaka 1998 na kisha kunyongwa hapo jana .

Pillay ambaye yuko ziarani nchini Mexico amesema kuwa amekasirishwa kutokana na sababu kuwa hata Gavana wa jimbo hilo hakuchuka hatua yoyote ya kusitisha hukumu hiyo. Pillay amesema kuwa Bwana Leal Garcia hakupewa ruhusa ya kuzungumza na ubalozi wa nchi yake kama raia wa kigeni kwa kuwa ilikuwa haki yake.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter