Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yaelezea kuwepo kwa uwekezaji wa kuridhisha kwenye miradi ya nishati mbadala ya umeme

Ripoti ya UM yaelezea kuwepo kwa uwekezaji wa kuridhisha kwenye miradi ya nishati mbadala ya umeme

Uwekezaji wa dunia kwenye miradi ya nishati ya umeme inayojali mazingira umeongezeka kwa kiwango cha asilimia 32 huku China na baadhi ya nchi za Ulaya zikichangia pakubwa kwenye ongezeko hilo. Kuwepo kwa matumizi ya nishati ya umeme wa upepo, na ongezeko la watumiaji wa mitambo ya uzalishaji umeme wa solar ni maeneo yaliyoleta mapinduzi hayo.

Katika ripoti yake mpya  shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limesema kuwa kwa mara ya kwanza nchi zilizoendelea zimeonyesha hatua ambayo inaanza kujibu maswali ya muda mrefu.Ripoti hiyo imeonyesha namna nchi kadhaa zilizozingatia kuongeza mafunga ya fedha ili kufadhilia miradi ya nishati mbadala ya umeme .Lakini pia ripoti hiyo imetaja ongezeko la asilimia 39 katika nchi za Amerika ya Kusin na ile ya Kati.